Friday, 8 April 2016

NAFSI SI HURU



Sheria nyingi za nini mwatunga, ilhali kwa kusudi  mwazivunja
Wanasheria na waheshimiwa yakiwemo, miongoni  mwa majina mengi mnayojiita
Eti yanatokana na baadhi ya mataji mengi wenyewe mnayojitwika
Umekua mtindo kuvunja sheria kwa kufanya fujo mikutanoni
Nami naikamata kalamu yangu kama tindo
Za Arudhi nazivunja kamwe sizingatii mitindo
Ila sio kusudi,  Yakuandika yamezidi mengi
Meli kisha ng’oa nanga, nasikitika sina muda
 Mezani basi sikai tena,eti nitosheleze mizani

Mengi maovu wayafanyayo, wanyafanya hadharani
Kwa kusudi watutiya tafarani Kila uchao mwingine wao,
 Mfisadi afichuliwa tena  miungoni mwao
Ungozi kwao viongozi, umekuwa kama mchezo
 Kulaumiana mbele ya umma, maskini anapo umia
Sina budi kusita kila mara katika uandishi wangu
Dakika moja kwa heshima za mashujaa babu zetu
Kwa imani, popote walipo, natumai wapo pema peponi
Wao waliojinyima kizalendo  zao nyoyo kazitoa vichakani
Kajikaza kisabuni, kusudi wajukuu tuishi pasipo mashakani
Laiti wangalijua, wasingali mfukuza mkoloni
Ninao ushahidi wa Mashujaa waliobaki mkononi
Haufichiki uchungu wanaohisi moyoni
Wanahudhuria sherehe za kusherekea uhuru kwa huzuni
Tayari nchi imenyakuliwa tena na majirani wetu
Kiongozi wetu ni rafiki yake kiongozi wa wanyakuzi
Sijui tuwalaumu akina nani safari hii
Wanaoiba asilimali ya umma twawaona magazetini
Ilhali maskini wasio na hatia wamejazwa gerezani
Hakika ni mengi myafanyayo, tuelezani za nani mwafuata nyayo



No comments:

Post a Comment